Mimi ni mmiliki wa eneo hili nimehamia mkoa mwingine na kujenga huko sasa natafuta wa kununua nihamishe kila kitu changu ninakoishi. Ni eneo ambalo lina nafasi kubwa na lipo kwenye mipango miji, limepimwa tangu mwaka 1990 na limepakana na taasisi mbalimbali. Kwa magharibi kuna shule ya msingi na kaskazini kuna kanisa la Wasabato na mashariki kuna barabara na kusini kuna msikiti hauko mbali. Ipo njia panda, kwani katikati ya kanisa kuna barabara inaelekea shuleni. Itafaa kwa biashara ya aina yoyote. Nauza kwa sababu nina mashamba ya kuendezwa kuliko. Ndiyo maana natafuta wa kuinunua. Mfano mtaa wote wa Ganana umezungukwa na ofisi za umma na nyumba za kuishi viongozi wa serikali na wakazi wengi. Kituo cha mafuta au kituo cha afya kingefaa pale. Karibuni, mimi ndiye mmiliki tangu mwaka 2002.