Aloe Vera Gel ni bidhaa ambayo inatengenezwa na Aloe Vera kwa Kutumia kiini cha ndani cha jani. Kinywaji hiki kina manufaa makubwa sana kwenye afya haswa kwasababu ya uwezo wake wa kusafisha mfumo wako wa mmeng’enyo wa chakula na hivyo kuongeza uwezo wa mwili kufyonza virutubisho kutoka kwenye chakula. Vile vile, seli nyingi za *kinga ya mwili* zinapatikana kwenye mfumo huu wa mmeng’enyo hivyo kwa kutumia Aloe Vera, kinga yako ya mwili itaimarika. Faida zingine za Aloe Vera ni kama; 1. Kuondoa taka mwili/sumu 2. Kuongeza nguvu. 3. Kusaidia kwenye vimbe. 4. Kusaidia kupata choo vizuri. 5. Kusaidia kwenye vidonda vya tumbo. 6. Kusaidia kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu. 7. Kuboresha mwonekano wa ngozi. 8. Kupunguza uchovu na maumivu.