Bill Counter model JN2040 ni mashine imara na ya kisasa kwa biashara yoyote inayopokea pesa taslimu kwa wingi. Ina uwezo wa kuchakata hadi noti 1,000 kwa dakika, hivyo inaharakisha kazi na kuondoa makosa ya kuhesabu kwa mikono. Ina stack capacity ya noti 200, kioo cha kuonyesha hesabu kwa 4 digits, pamoja na batch display kwa kuhesabu mafungu kwa usahihi. Mashine hii inakubali noti za ukubwa tofauti (50×110mm hadi 90×170mm) na thickness 0.075–0.15mm. Inatumia AC 220V / 50Hz na wattage ya 80W, hivyo ni ya matumizi madogo ya umeme. JN2040 ni chaguo bora kwa maduka, ofisi, supermarkets, benki ndogo na biashara zinazotaka kasi, wepesi na usahihi bila usumbufu.