Digital clamp meter ni kifaa cha kupimia umeme kinachotumika kupima mkondo wa umeme (current), volti na upinzani bila kukata waya. Kina sehemu ya kubana (clamp) inayoshika waya na kutoa kipimo kwa njia ya kidijitali kwenye skrini. Hutumika sana na mafundi wa umeme.