Suti hii imeshonwa kwa mtindo wa kisasa wa 'Slim Fit' unaokaa vizuri mwilini. Rangi yake ya kahawia iliyokolea ikichanganywa na mistari ya dhahabu/cream inaleta muonekano wa kitajiri na nadhifu sana, unaoendana kirahisi na mashati ya aina mbalimbali.